
MTI WANGU
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Mh. Paul Makonda amezindua program ya kupanda miti kwa lengo la kuboresha na kuhufadhi mazingira (ijulikanayo kama MTI WANGU). Katika uzinduzi wa program hiyo vijana wa skauti mkoa wa Dar es salaam nao walishiriki kumuunga mkono Mh. Mkuu wa Mkoa Paul Makonda lakini ikiwa ni moja ya shughuli za skauti katika kutunza mazingira kupitia program ijuluikanayo kwa jina la Programu ya Dunia ya Mazingira "World Enviroment Program".