
SKAUTI WACHANGIA DAMU KONDOA
Kupitia maadhimisho ya miaka mitatu ya uskauti kondoa, ambayo ilianzishwa rasmi mnamo tarehe 15/07/2014 kiongozi wa skauti wilayani humo aliweza kuandaa utaratibu wa kutoa huduma kwa jamii kwa kuwaandaa vijana wake kujitolea damu na kuwasaidia Mama wenye ujauzito kwa kipindi cha kujifungua, wagonjwa mbali mbali watakao hitaji damu kwa wakati husika.
Niliwahamasisha Vjana wangu juu ya uchangiaji wa damu maana mi nimekuwa nikitoa mara kwa mara. Pia walipewa elimu na wataalamu. Lakiniwalichangia damu kwamadhumuni ya kutimiza kanuni ya 3, ya 4 na ya 6 za skauti. Pia ilitolewa taarifa ya kua Mama wajawazito, wagonjwa na majeruhi wengi kufariki dunia kwa ukosefu wa damu ndio wakaamua kujitolea Damu ili kuokoa maisha, lakini pia ulikua nimpango maalumu walio jipangia skauti wa Kondoa kujitolea damu.
Tukio hili lilifanyika katika hospitali ya wilaya kondoa, ambapo ndio hospitali kuu ya rufaa hapo Kondoa kiujumla zoezi la uchangiaji Damu lilikua zuri maana Vijana wengi walishiriki na walitamani kufanya tendo hilo jema mara kwa mara pindi ikihitajika. Aidha iongozi wa skauti kondoa alitoa rai kwa jamii kuwa ijitolee kusaidia watu wenye uhitaji wa damu maana damu si kam bidhaa nyingine ambazo zinauzwa sokoni au dukani, Jamii iondokane na imani kuwa ukitoa damu utapata matatizo au utaugua, "Mi ni mfano mzuri tu nimeshachangia Damu mara 13 na hakuna tatizo lolote ambalo nimepata zaidi naona napata faida", lakini pia unapata fursa ya kujua afya yako kwa kupima magonjwa ambayo ni hatari kama vile UKIMWI, ugonjwa wa Ini, magonjwa mbalimbali na hata kujua grupu lako la damu yako.