SIKU YA AMANI DUNIANI 21 SEPTEMBA 2017

SIKU YA AMANI DUNIANI 21 SEPTEMBA 2017

Habari Rafiki. Kwa mujibu wa kalenda leo ni 21 Septemba "Siku ya Amani Duniani" haimaanishi siku nyengine ni siku za kuvuruga au kuto dumisha Amani. Bali siku hii imewekwa maalum kwaajili ya kuhubiri, kutangaza na kuhamasisha Amani ulimwenguni, nchini Tanzania tutaadhimisha sherehe hizi za siku ya Amani kiTaifa Mkoani Dar es Salaam siku ya Jumamosi tarehe 23 Septemba katika viwanja vya muembe Yanga wilaya ya Temeke, maadhimisho hayo tata ambatana na matembezi ya kuhamasisha Amani kuanzia Maeneo ya kituo cha polisi Chang'ombe (Maarufu Usalama) kueleza viwanja vya muembe Yanga na Mgeni Rasmi kwenye sherehe / maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Siro. Event itaanza saa mbili kamili asubuhi na kuisha saa sita mchana, kila mmoja ni mdai wa Amani (Tunaamini Amani Husna kwa mtu binafsi then kwa wengine) hivyo tunawaalika rasmi kushiriki kwa pamoja ili tufikie malengo. KAULI MBIEU: PAMOJA KATIKA KUDUMISHA AMANI: HESHIMA, USALAMA UTU KWA WOTE. Kwa mawasiliano piga 0653373432 (wasap)

Share via

Share