Sherehe za Miaka 100 ya uskauti Tanzania

Sherehe za Miaka 100 ya uskauti Tanzania

BAADHI YA MANENO ALIYOONGEA MAKAMU WA RAIS KWA NIABA YA MLEZI WETU RAIS JOHN POMBE MAGUFULI Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo alimuwakilisha Mlezi wa Chama cha Skauti Tanzania ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt John Pombe Magufuli katika uzinduzi wa sherehe za miaka 100 za Skauti nchini Tanzania. Katika hotuba aliyoisoma kwa niaba ya Rais, Makamu wa Rais amewapongeza Skauti Tanzania pamoja na viongozi wao kwa kutimiza miaka 100 na kuendelea kujenga na kulea maadili mema na kupambana na mmomonyoko wa maadili katika jamii yetu. Akisoma hotuba hiyo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamu wa Rais alisema " Mimi mlezi wenu nitajisikia vyema kufanya kazi nanyi katika kuwajenga vijana wetu kwa maarifa, kuwalea katika misingi ya kizalendo,kuwaelekeza kujiamini ili hatimaye kujenga Taifa la Vijana wema kadri inavyowezekana". Kwa bahati nzuri chama hiki kimesukwa na Wazee na Vijana wenye hekima na busara katika kulinda mila na desturi zetu njema. Aidha, aliwashukuru na kuwapongeza Marais Wastaafu waliotangulia kuwa Walezi wa Skauti Tanzania Bara na Zanzibar Wakati tunapata uhuru mwaka 1961 chama hiki kilikuwa na wanachama wapatao 850 na sasa kinawanachama milioni nne. Nafahamu Skauti wanachangamoto zao ambazo zinaweza kutatulika kupitia Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuangalia uwezekano wa kuwapatia ofisi ili kazi zifanyike kwa ufanisi, kwa Maafisa Ardhi wa Mikoa na Wilaya kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli zao, kwa Wakuu wa Vyuo, Shule za Sekondari na Shule za Msingi, Taasisi za Dini, kuzingatia waraka wa wizara ya elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi kuhusu kazi za ziada. Makamu wa Rais pia alisisitiza kuanzishwa kwa miradi ambayo itawashirikisha vijana kujiinua kiuchumi na kukabiliana na ukosefu wa ajira. Mwisho, Makamu alitoa wito kwa wazazi kuwaruhusu vijana kujiunga na kundi zuri la chama cha skauti Tanzania.

Share via

Share