NILICHOJIFUNZA KWENYE KAMBI YA SIKU YA SKAUTI AFRICA
Habarini za mda huu ndugu zangu popote mlipo,napenda kuchangia nanyi kile nilichojifunza kwenye siku ya Afrika iliyofanyika nchi Tanzania,katika mkoa wa Arusha,eneo la Kisongo.
Yafuatayo ni machache kati ya mengi niliyojifunza;
1:UPENDO/LOVE
-Kambi hii imeonysha upendo ni kitu muhimu sana kati ya mtu na mtu,mtu na mazingira yake na mtu na nafsi yake,kambi hii imejumuisha watu kutoka mataifa mbalimbali na mabara mbalimbali kama vile Afrika,Asia na Ulaya,lakini watu tumeishi kwa upendo mkubwa bila kujali tofauti za mataifa na mabara yetu,hili ni jambo la kufurahisha na lenye upendo wa halo ya juu kabisa.
2:UMOJA/UNITY
-bila kuzingatia tofauti za umri,matabaka na mataifa yetu,kila jambo lililofanyika limefanyika kwa ushirikiano mkubwa sana,maamuzi yamefanyika bila kujali mataifa na matabaka ya watu,jambo hili nadhani lipo ndani ya skauti pekee.
3:AMANI/PEACE
-Kumekuwa na Amani ya hali ya huu kabisa maadhimisho haya ya siku ya Skauti Afrika,hakuna jambo lolote baya lililolipotiwa kutokea,jambo kama hili ni nadra sana kutokea katika maeneo yenye mjumuiko mkubwa wa watu kama hapa.Skauti wiiii!!!
4:NIDHAMU/DISCIPLINE
Katika maadhimisho haya ya siku ya Skauti Afrika, kumekuwa na nidhamu ya hali ya juu sana kutoka kwa washiriki.watu wameishi kwa mujibu wa kanuni na taratibu za Skauti,ni jambo lenye kupendeza sana.
Hayo ni baadhi tu niliyopenda kuchangia nanyi katika siku hii ya maadhimisho ya siku ya Skauti Afrika.