SKAUTI NA UTOKOMEZAJI WA PLASTIKI BAHARINI
1. Changamoto zilizopo katika mazingira ya bahari ya kuwa na uchafuzi mkubwa wa plastiki
2. Kupungua kwa uchumi kwa watu wanaotegemea bahari kufanya shughuli zao
3. Athari kwa viumbe wa majini kuonekana wakiwa wamekufa pembezoni mwa bahari
4. Athari ya mabadiliko ya tabia nchi
5. Athari kwa afya za watu wanaotumia viumbe wa majini
6. Ukosefu wa elimu kwa watu juu ya maendeleo endelevu ya dunia
7. Mwamko mdogo wa vijana wa skauti katika kuikomboa jamii wanayoishi kupitia shughuli za skauti
1. Nilianza kwa kutoa elimu kwa skauti juu ya utokomezaji wa PLASTIKI BAHARINI
2. Nikaomba msaada wa serikali ili kuwapata wavuvi pamoja na watu wanaotegemea bahari kufanya shughuli zao
3. Kisha nikatumia skauti kufikisha ujumbe na kuchukua hatua ya kufanya usafi pembezoni mwa bahari.
4. Nikatumia mitandao ya kijamii kama Instagram kufikisha ujumbe kwa watu wengi hususan vijana
5 Nilifundisha vijana wa skauti katika jukwaa la vijana wa skauti Tanzania kuhusu madhara ya plastiki
Mradi huu unafundisha watu juu ya kutunza mazingira ya bahari kwa kupunguza matumizi makubwa ya PLASTIKI BAHARINI.
Pia unafundisha jamii ya watu juu ya athari zitokanazo na utunzaji hafifu wa mazingira ya bahari.
Mradi huu umelenga kuikomboa jamii ya sasa na ya baadaye juu ya mazingira ya bahari na rasilimali zote zipatikanazo humo kunufaika Nazi.
Mradi huu unafundisha kuwa skauti tunao mchango mkubwa sana katika kuibadili jamii yetu na Dunia kwa ujumla