SKAUTI NA ELIMU YA AFYA YA UZAZI
1. Changamoto zinazowakumba vijana kuhusu afya ya UZAZI.
2. Ukosefu wa elimu ya afya ya uzazi kwa jamii.
3. Ongezeko la magonjwa ya afya ya uzazi kwa watu.
4. Athari hasi za mahusiano salama na yanye heshima kwa vijana .
5. Mwamko mdogo wa vijana juu ya huduma rafiki kwa vijana.
1. Nilianza kutafuta msaada kutoka kwa halmashauri ya wilaya ya Kilwa kitengo cha afya ili tuweze kupatiwa elimu kwa kina kuhusu afya ya uzazi.
2. Skauti tukapokea elimu ya afya ya uzazi kutoka kwa muuguzi mkuu wa wilaya.
3. Skauti tukatumia elimu hiyo kuwafundisha vijana hususan wanafunzi ambao ni jamii inayoelekea kupotea kama wasipopatiwa elimu hiyo ya afya ya uzazi.
4.Nikaanzisha kikundi cha watu maalumu ambao watahusika na kujadili kuhusu afya ya uzazi na kutatua changamoto zinazowakumba.
1. Mradi huu unafundisha vijana namna ya kutunza afya zao za uzazi na thamani ya afya ya uzazi kwa maisha ya leo.
2. Mradi huu unaongeza mahusiano salama na yanye heshima kwa vijana kwa maendeleo yao.
3. Mradi huu unapunguza athari zitokanazo na ukosefu wa elimu ya afya ya uzazi.
4. Mradi huu unaokoa kizazi cha sasa na cha baadae kwa kutunza afya zao za uzazi.
5. Mradi huu unaongeza mwamko wa vijana juu ya huduma rafiki kwa vijana